Kuwanga serious kizee.
Unadai ule Salim wa veve base ni mharamia? Kwa nini?
Kwa sababu yeye ni Msomali na ni Muislamu?
Salim ameishi kwa hii mtaa tangu enzi.
Na vile Salim hukuunganishia surba ya veve na njugu hata ukisota.
Kanashika mara dat dat na unapata mpango Sunday.
Buda kuwanga serious. Naskia wewe ni fala, ulidhani Ras Kamboni ni base ya wanati wa Somalia
Mresh achanga za ovyo
Juzi umeandika kwa Facebook vile unagwaya Wasomali.
Unadai hawa wasee ni ma Al Shabaab ki undercover,
Alafu boi Mkisii anapatikana na mabonoko na makombora kwa keja Kayole,
Haja gani kuchukia wasee ju wanaishi Eastleigh.
Kaa mat za kwenu zimechapa basi si uhamie Buru?
Wachanga kujipandisia. Ujinga ni dame kuita shonde “human cow-dung” eti ju amesoma.
Wasee inafaa tu sare kuwa vigeugeu.
Hii stori ya kushuku wasee bila sababu ni muhadhara aisee,
Kumbuka PEV venye watu walichinjana na manjora na kuchoma makanisa,
Na before hawa watu walikuwanga maneiba wa kusaidiana chumvi na nare.
Si tukuwe serious this time tuchuje siasa za kikabila?
But first, Wasapere waseme“Siendi shop kwa sababu Al shabaab wamesababisha mambo ya kustaajabu”
Wasapere, Wajaka, Wakale, WaIngo na Wakenya wote gotea hii stori.
By Michael Mungai